WANAFUNZI
WA KIKE WATUMIA MTANDAO KUJIUZA
PENGINE
haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi.
Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi,
lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi
wa gazeti hili umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya
kijamii yamechochea ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya
na zaidi biashara ya ukahaba vyuoni.
Mitandao
ya ‘Facebook’, ‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza
kuwaunganisha watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
Mwananchi
Jumapili limebaini kuwa katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa
yakiwa na malengo tofauti.
Baadhi
wameanzisha makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara, kidini,
michezo, burudani, vichekesho na mengine ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote
anaweza kujiunga na kuona kinachoendelea ndani.
Mbali
na hayo ndani ya mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha
biashara ya ukahaba, yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali nchini.
Uchunguzi
umebaini kuwa wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao
wameweka picha na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na
bei waliyoweka.
Baadhi
ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho
la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine
katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia
katika mitandao ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa
makundi yaliyoundwa kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba
za simu za wahusika, zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha
na kuvutiwa, unaweza ukapiga simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano
kabla ya kukubaliana.
Uchunguzi
wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka
chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao
hiyo.
Baadhi
ya vyuo wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye
mitandao ni pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha
Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya
Biashara (CBE) na Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Kwa
nyakati tofauti, waandishi wa gazeti hili walitembelea makundi yanayojinadi
kufanya biashara hiyo pamoja na kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao
waliweka picha na namba zao kwenye mtandao.
Wasichana
hao walijitambulisha kwa majina, vyuo na vitivo wanavyosoma na baada ya
kuwafuatilia kwa kuweka ahadi za kimapenzi ilithibitika kuwa wanafanya biashara
ya ukahaba huku wakiwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Mmoja
wa wasichana hao alijitambulisha kwa jina la Bianca (sio jina lake halisi),
ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa pili Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
Baada
ya mwandishi kufanya naye mawasiliano walikubaliana kukutana eneo la Udasa na
muda wa ahadi ulipofika, mwandishi alifika eneo hilo na kukutana na binti huyo
ambaye aliiona picha yake na namba ya simu kwenye mtandao, tofauti na
alivyodhani awali kuwa huenda wasichana hao wanatumia picha za watu wengine
kujinadi.
Kutokana
na lengo la msichana kuwa ni biashara ya ngono, mwandishi wa gazeti hili
alilazimika kumpeleka binti huyo katika hoteli moja maarufu jijini, akimweleza
kuwa inabidi wanywe pombe kwanza kabla ya kwenda chumbani kwa makubaliano ya
kumlipa Sh50,000.
Binti
huyo alikabidhiwa fedha hizo ili kumwaminisha uhalisia wa kuwapo hitaji na muda
wa kwenda naye chumbani ulipofika waliongozana lakini mwandishi akatoroka
njiani akiwa amethibitisha kuwapo kwa tabia hiyo.
Gazeti
hili lilimfuatilia mwanafunzi mwingine ambaye alijitambulisha kuwa anasoma
katika Chuo cha Ustawi wa Jamii, ambaye kama ilivyokuwa kwa wa kwanza, hakupata
taabu kujieleza.
Baada
ya mwandishi kueleza alipoipata namba yake mazungumzo yao yalikuwa hivi:Binti
aliuliza: “...Kwa hiyo, uko wapi?”Mwandishi alijibu: “Nipo Ubungo.”Binti
akauliza tena: “Unaweza kuja Ustawi?”
Baada
ya mawasiliano hayo mwandishi aliambiwa binti huyo kuwa anaweza kumfuata chuoni
hapo.
Mwandishi
wa gazeti hili alifika maeneo ya Kijitonyama jirani na kilipo chuo hicho, na
kumpigia simu binti huyo, ambaye aliipokea na safari hii alimwambia mwandishi
kuwa ikiwezekana aje na rafiki yake.
Ilichukua
nusu saa kwa wasichana hao kufika katika baa, ambayo mwandishi alikaa
kuwasubiri, mara walitokea wasichana hao wakiwa wachangamfu, warembo waliovalia
mavazi ya kisasa, yaliyoacha sehemu kubwa ya miili yao wazi.
Muda
wa dakika saba walizokaa zilitosha kuwafanya wazoeane na mwandishi kama vile
waliwahi kukutana miaka mingi ya nyuma, stori, vinywaji na mambo
yalifanyika kama ilivyokuwa Udasa.
Mwananchi
Jumapili liliendelea na uchunguzi wake kwa wasichana wengine ambao wameweka
picha zao katika mitandao hiyo wakijiuza, ambapo walipopigiwa simu walijibu na
kufika katika maeneo waliyokubaliana.
Gazeti
hili liliwasiliana na wasichana zaidi ya 10 kutoka katika vyuo tofauti jijini
na wote walikiri kuwa wapo katika biashara wakieleza kuwa mteja akipatikana
wanaweza kukubaliana malipo.
Wasichana
hao ni tone kati ya mamia ya wanafunzi wa vyuo, ambao hivi sasa wamebuni njia
hiyo baada ya kuona ule mtindo wa kujiuza nyakati za usiku katika maeneo
mbalimbali kuwa umeanza kupitwa na wakati.
Baadhi
ya wasichana wanaofanya biashara hiyo hasa mkoani Dodoma, wamekuwa wakiwatumia
mawakala ambao huwapa namba za simu na pindi anapotokea mteja, huunganishwa na
kiongozi wa kikundi hicho kabla ya kupata aina ya msichana anayetaka.
Hata
hivyo mteja asiporidhika na msichana aliyeletewa, hutafutiwa mwingine, huku pia
wasichana husika wakitofautiana mahitaji kabla ya kufanya nao ngono.
Wapo
wanaoweka masharti ya kunyweshwa pombe kwanza, kupelekwa disko au kwenye muziki
pamoja na wanaokwenda kwa matakwa ya mteja moja kwa moja.
Wanafunzi
wazungumza
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti na Mwananchi Jumapili baadhi ya wanafunzi walikiri kuwa
katika vyuo kuna wasichana wanaojiuza, ingawa walisema kuwa, hawajui kama
wamefikia hatua ya kuweka picha katika mitandao na namba za simu.
Mwanafunzi
Aisha Idd wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), alisema kuwa biashara ya
ukahaba inafanyika, lakini hafahamu kama wanatumia mitandao kujitangaza.
“Sijawahi
kufikiria kama wanaweza kufika mbali kiasi hiki, sijui kama wanajiuza kwenye
mitandao, lakini hii inaonyesha kuwa tunakoelekea ni kubaya zaidi kwani hawa
ndio watu wanaotegemewa katika ujenzi wa taifa,” anasema Aisha na kuongeza:
“Ninafikiri
Serikali inapaswa kuliangalia hili, yaani wasomi ndiyo wanaoongoza kwa kufanya
mambo machafu, hii ni aibu na inaweza kuitia doa sekta nzima ya elimu
ionekane haina maana kama msomi wa chuo kikuu anaweza kufanya upuuzi huu.”
Naye
John Mkongo alisema kuwa hashangai kusikia kuwa wanafunzi hao wametafuta njia
nyingine ya kutafutia wateja kwa kuwa wanaweza kufanya chochote ili wapate pesa
za kufanyia starehe.
“Hii
inawezekana kabisa kwani hawa dada zetu wamefikia kufanya mambo ya ajabu kama
vile wamepata wazimu, ili kupata pesa wanaweza kukubali kufanya chochote, najua
siku za usoni tutaendelea kusikia mambo ya ajabu zaidi kwani hawa wenzetu
wamejitoa mhanga,” anasema Mkongo.
Anaongeza
kuwa kinachowafanya wasichana hao kujiingiza katika biashara ya ukahaba ni
tamaa, akitoa mfano baadhi ya wasichana ambao hawajihusishi kabisa na mambo
hayo.
“Mimi
ninaona kinachowagharimu hawa dada zetu ni tamaa tu, huku wengine wakiponzwa na
ulimbukeni wa kuvamia mambo, ambayo wameanza kuyaona baada ya kuingia chuoni
hasa kupenda vitu vya gharama kama vile simu, nguo, manukato na magari,”anasema
Mkongo.
Wakuu
wa vyuo wanena
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Profesa Tolly Mbwete anasema hali hiyo
inatokana na kukua kwa utandawazi.
“Ni
wakati sasa kwa wizara inayohusika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na
Michezo ) kuhakikisha inafuatilia jambo hili na kuchukua hatua stahiki,”
anasema Profesa Mbwete na kuongeza:
“Elimu nayo inatakiwa kutolewa kwa watumiaji ili kutokuathiri dhamira ya kukua kwa utandawazi, jamii nzima ielimishwe kuhusu matumizi sahihi ya mitandao hiyo.”
“Elimu nayo inatakiwa kutolewa kwa watumiaji ili kutokuathiri dhamira ya kukua kwa utandawazi, jamii nzima ielimishwe kuhusu matumizi sahihi ya mitandao hiyo.”
Naye
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma, Profesa Idris Kikula, anasema kuwa hana
taarifa za kuwapo kwa makundi hayo lakini akabainisha kuwa unatakiwa kuwapo kwa
utafiti ili kujiridhisha kama ni kweli hao wanaofanya hivyo ni wanafunzi wa
vyuo.
Anasema
kama yapo ni wakati sasa wa kuhakikisha wanakemewa kwani kuna baadhi ya wasichana
wanatumia mitandao kujitambulisha kuwa ni wanafunzi wa vyuo, wakati siyo
wanafunzi.
“Hapa
Dodoma katika kipindi cha Bunge wanawake wanaojiuza huwa wengi kila
unayemuuliza atakwambia anasoma chuo, lakini ukimuuliza kozi gani atakwambia
bado sijapangiwa hivyo hii ni hatari,” anasema Profesa Kikula.
Wazazi
wasikitika
Mkazi
wa Mbagala jijini Dar es Salaam, Florence Baltazar anasema vitendo hivyo
vinatokea kwa sababu ya kuiga mambo ya nchi za nje.
Baltazari
anasema Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inatakiwa kuhakikisha
inafuatilia mitandao hiyo ikibidi kuifunga kabisa.
Zubeda Hamza anasema vijana wa siku hizi hawajitambui hususan wasichana ambao wamekuwa hawapo makini na utu wao.
Zubeda Hamza anasema vijana wa siku hizi hawajitambui hususan wasichana ambao wamekuwa hawapo makini na utu wao.
“Kweli
kama msichana anajitambua hawezi kutongozwa katika mtandao na kukubali haraka
au kujinadi hivyo wasichana wanatakiwa kutambua utu wao,”anasema na kuongeza:
“TCRA
inatakiwa kuwa inafanya mapitio ya mitandao yote ili ile inayokiuka taratibu
waweze kuifungia.”
Kwa
upande wake Charles Mashiri anasema kuwa wasichana wa siku hizi wamekuwa
hawashikiki, hasa wanapofika vyuoni na kwamba hawataki kukaripiwa au kuonywa.
“Akiwa
nyumbani anakuwa mtaratibu lakini akitega mgongo kutoka kutoka nyumbani anaanza
tena ujinga wake, hivyo kama vitendo hivyo vipo basi Serikali inatakiwa
kufuatilia na kuchukua hatua zaidi,”anasema.
Mwananchi
Jumapili Februari
3, 2013
No comments:
Post a Comment