PARENTING/MALEZI



WATOTO WALIWA NA FISI, WAFA

Bahi. Watoto wawili wenye umri wa kati ya miaka miwili na mitano wameuawa na fisi katika Kijiji cha Mnkola, Kata ya Ibihwa wilayani Bahi Mkoa wa Dodoma katika matukio mawili tofauti.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Teya Kata ya Ilindi wilayani hapa, Paul Mwaja alisema kuwa watoto hao wameuawa katika matukio mawili ndani ya kipindi cha wiki moja.
Mwaja alisema tukio la kwanza lilitokea juzi ambapo mtoto mmoja wa kiume mwenye aliuawa na fisi wakati akiwa na wenzie wawili wamelala. “Alikwenda fisi katika eneo hilo na kumvuta (mtoto mmoja) na kumtafuna hadi akamuua,”alisema Mwaja.
Alisema usiku wa kuamkia jana, fisi huyo alirudi tena katika kijiji hicho na kumnyang’anya mama mmoja mtoto wake mdogo mwenye umri wa miaka miwili.
Mwaja alisema fisi huyo alimla mtoto huyo na kumbakisha kichwa na utumbo tu, hali iliyozua taharuki katika kijiji hicho.
Hata hivyo, alisema baada ya tukio hilo wananchi waliamua kufanya msako na kumkamata fisi huyo na kumuua.
Baba mzazi wa mtoto aliyeuawa usiku wa kuamkia jana aliyejitambulisha kwa jina moja la Mchamingi, alisema hawana imani kama fisi huyo kama ni wa kawaida kwani katika tukio la kwanza kabla ya kuuawa, alikimbilia katika kijiji jirani cha Bahi Makulu na kupotelea kwenye nyumba za watu.

CHANZO: Mwananchi: Juni 27,  2015




DISCIPLINING A CHILD
 Disciplining a child is not easy for the child - or the parent. But correction with love produces character qualities that will eventually bring to both parent and child.

Pray for godly wisdom to properly discipline your children if you are a parent or guardian. If you are not one of those get ready for it.

 
WANAUME NENDENI KLINIKI MTAMBUA AFYA ZA WAKE ZENU`
Na Mwandishi wetu
17th March 2013

Wanaume wameshauriwa kushiriki kliniki ili waweze kutambua afya za wake zao wanapokuwa wajawazito badala ya kuwatelekeza.
Ushauri huo ulitolewa jana na Meya wa manispaa ya Dodoma, Emanuel Mwiliko, wakati alipokua akifungua kambi ya kupima afya kwa akina mama na watoto mjini hapa.
Mwiliko alisema kuwa kumekuwapo na tatizo kubwa kwa wanaume wengi nchini kuwa wazito kwenda kliniki hali inayosababisha wasiweze kujua afya za wake zao wanapokuwa na matatizo.
Alisema kuwa ifike wakati wanaume wabadilike kutoka katika mtazamo walio nao hivi sasa na kuanza kushiriki kuwapeleka wake zao kliniki ili waweze kuzitambua afya za wenzi wao.
“Sisi akina baba tumekuwa mstari wa nyuma katika kushiriki kliniki hivyo natoa wito tujitokeze katika kushiriki kliniki sisi na wake zetu hali ambayo itatusaidia kujua afya zao zinaendeleaje,” alisema Mwiliko.
Aidha alitoa wito kwa jamii kuwa karibu na akina mama wajawazito ili kuhahakisha kuwa wanajifungua salama.
“Tuhahakishe kuwa tunafuatilia afya za akinamama wajawazito kabla na baada ya kujifunga ili kuweza kuwasaidia katika kuwalea watoto wao katika afya iliyo njema,” alisema.
Naye meneja wa hospitali ya Agha khan mkoani hapa ambao wameandaa kambi hiyo ya kupima afya bila malipo kwa wananchi, Kibe Abel, alisema kuwa lengo ni kuwasogezea wananchi huduma karibu.
Abel alisema kuwa huduma hizo zinatolewa kupitia mradi wa tuunganishe mikono katika kuboresha afya ya mama na mtoto (JHI) kwa ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Canada (CIDA).
“Huduma tunazo zitoa ni kupima watoto na akimama wajawazito pamoja na kutoa elimu jinsi gani akina mama wanaweza kunyonyesha na namna ya kuwalea watoto wao katika afya nzuri,” alisema Abel.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

 
WATOTO 4,485 WAZALIWA NA VICHWA VIKUBWA
Na Jimmy Mfuru

7th March 2013

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi
Serikali imesema watoto 4,485 nchini wanazaliwa na vichwa vikubwa tatizo ambalo  linalosababishwa na kujaa maji  kichwani na matundu kwenye uti wa mgongo.
Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hussein Mwinyi, alipokuwa akipokea msaada wa mashine mbalimbali kwa ajili ya upasuaji wa watoto hao  zilizotolewa na Saudi Arabia.
Aidha, Dk. Mwinyi alisema kwa wastani watoto 250 kila mwaka huzaliwa na tatizo hilo hivyo msaada huo utasaidia kurahisisha upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili  Taasisi ya Mifupa (MOI).
Alisema mashine zilizotolewa ni CT-Scan na mashine ya Ultra Sound na vifaa vingine vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 140,000 (Sh. milioni 224).
Aliongeza kuwa wingi wa watoto wanaozaliwa na tatizo hilo unatokana na kuchelewa kupelekwa hospitalini  kwa sababu ya umaskini wa familia zao.
Balozi wa Saudi Arabia nchini, Hani Monima, alisema nchi yake imeguswa na ugonjwa wa watoto hao ndio maana imetoa msaada huo
Mkurugenzi wa MOI, Dk. Lawrence Maseru, alisema huduma za upasuaji wa vichwa vya watoto zilikuwa duni kutokana na uhaba wa vifaa sasa zitatolewa kwa ufanisi zaidi.
CHANZO: NIPASHE

RAISE UP A CHILD
Luke 15:11-32 (NIV)
4       Key parenting principles from this parable of the lost son
The father models several key PARENTING principles that reflect the HEART of God.
Lesson 1 for parents: The father allowed his son to make CHOICES.         Deut. 30:15-20
What kind of parent am I? Warnings for Us
•        Without CHOICES children grow up to be IMMATURE.
Lesson 2 for parents: The father allowed his son to experience CONSEQUENCES.                Galatians 6:7-10
What kind of parent am I? warnings for us
•        Without CONSEQUENCES children grow up to be IRRESPONSIBLE.
Lesson 3 for parents The father received his son with COMPASSION.
•        What kind of parent am I?
•        Without COMPASSION children grow up to be IRATE.
Lesson 4 for parents: The father answered his son with CONVICTION.
•        What kind of parent am I?
•        Without CONVICTION children grow up to be INSECURE.
What kind of parent am I?
Summary for parenting principle
1.      Without CHOICES children grow up to be IMMATURE.
2.      Without CONSEQUENCES children grow up to be IRRESPONSIBLE.
3.      Without COMPASSION children grow up to be IRATE.
4.      Without CONVICTION children grow up to be INSECURE.





RISE UP AGAINST VIOLENCE AGAINST WOMEN & CHILDREN!  
The growing national crisis of sexual violence against women and children in SA has dominated the media since the horrific rape and murder of 17 year old Anene Booysen in the W/Cape.
Social studies have emerged making South Africa the world leader in sexual violence and domestic abuse against women. Something is terribly wrong with SA society – and urgent action is required.
I am also deeply concerned that despite all the public discussion about this horrendous scourge in our nation, the Christian Church has chosen to remain mostly silent and disengaged.
When more than 64000 women are raped and 2400 are murdered every year in a nation, and when 25000 children are raped – some as young as 10 months old – we have to acknowledge we have a serious spiritual crisis in SA. The moral breakdown in SA is the result of spiritual darkness.
And while the nation reels against this brutal onslaught against women and children, Top TV is forging ahead with its plans to launch three 24-hour porn channels in South Africa.
On 14 Feb “Watchmen on the Wall” covered the opening of Parliament (broadcast on Tues 19 Feb on TBN Africa at 7pm). We spoke to political leaders and cabinet ministers about the challenges confronting SA. I also spoke to COSATU’s Zwelinzima Vavi, about Top TV’s application.
Apparently, Vavi was unaware of Top TV’s second application to launch 3 porn channels in SA and indicated that Top TV betrayed COSATU. The trade union is an investor in Top TV.
ICASA will hold public hearings into Top TV’s application on 14 March 2013 at their HQ in JHB. Please email Norman at ngidi@icasa.org.za to request a slot to make your submission.
God is opening significant doors for Family Policy Institute to advance His kingdom in the corridors of power. I am constantly aware that the Lord is in complete control of this ministry.
‘Watchmen on the Wall’ was granted an exclusive interview with Chief Justice Mogoeng Mogoeng on 14 Feb. The Chief Justice spoke candidly about his faith in God and the opposition against him.
My interview with the Chief Justice of SA will be broadcast on TBN Africa on 12 March at 7pm.
I am planning a 10 000 men march against sexual violence against women and children soon. I plan to invite leading men in society to publically speak out against this scourge. We will also hand a list of urgent demands to Government, which if implemented will dramatically reduce these crimes.
The Christian Church must lead in the fight against violent attacks on vulnerable women and children.
Family Policy Institute is currently fighting many critical battles on various fronts. Sometimes the battle seems overwhelming. But I thank God for His strength and your prayers and support.
We are gearing up to fight some major battles for the family and for Biblical values in SA. But we cannot do this without your help. Will you please consider partnering with FPI in this vital ministry.
You can partner with me via a financial contribution directly into FPI's banking account. Your contributions helps keep me on the frontlines of the battle to defend faith, family & freedom.
You can also make a generous once-off donation to FPI to support our vital work. As a registered Public Benefit Organisation (PBO) with SARS your contributions to FPI are tax-deductible.
Tax certificates are available on request by emailing: anaidoo@familypolicyinstitute.com
Please help me defend the family and advance your Biblical values where it matters most.
Standing
Errol Naidoo

.source : family policy institute



unsubscribe

forward

print pdf






YATIMA ABAKWA KWENYE DANGURO DAR MIAKA 10
Na Romana Mallya
16th February 2013

*    Alawitiwa na kuambukizwa virusi vya ukimwi
*    http://www.ippmedia.com/images/frontend/headline_bullet.jpg  Polisi naye adaiwa kumbaka akiwa kituoni

Nyumba inayodaiwa kutumiwa kama danguro ipo Mwananyamala Magengeni jijini Dar es Salaam.
Msichana yatima, mkazi wa mkoani Manyara, amefungiwa kwenye danguro  kwa zaidi ya miaka 10 akinyanyaswa kingono, kuteswa na kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi  (VVU).
Msichana huyo aliyeondolewa nyumbani kwao Oysterbay mjini Babat,i alilaghaiwa na mwanamke aliyejifanya kuwa msamaria mwema, akitangaza  nia ya kumsaidia kielimu na kimaisha, kufuatia kifo cha mama yake mzazi.
Msichana aliyefikwa na masahibu hayo ni  Sara Tarimo (27) ambaye aliangukia mikononi mwa  mwanamke mwenye danguro hilo, Abia Lucas (44) anayeishi Mwananyamala Magengeni.
Ilikuwa ni baada ya kifo cha mama yake  Magreth Kitinati, aliyekuwa akiishi naye  Oysterbay huko Manyara. Sara anasema mwanamke huyo alimtoa kijijini kwao hadi jijini Dar es Salaam, na kumshinikiza kwenye `utumwa wa ngono’ kwa kipindi cha miaka 10 akiwa amefungiwa ndani.
Akiwa mwanafunzi wa shule ya msingi, mama yake mzazi alifariki, hivyo ujio wa msamaria huyo ulikuwa faraja na tumaini jipya kwa maisha yake. Haikuwa hivyo. Sara alisema  alipoteza bikra yake baada ya kumlazimisha kufanya ngono  na mwanamume mtu mzima, aliyembaka na ukawa mwanzo wa kutumiwa kingoni na wanaume wa kila aina. Sara alisema alifanywa unyanyasaji huo akiwa na miaka 13 na kwamba hilo lilikuwa   tukio lake la kwanza kukutana na mwanaume. Baada ya kufanikiwa kutoroka na kuwataarifu polisi nyendo za mama huyo ambaye sasa anashikiliwa kwa mahojiano, Sara anasimulia kumbukumbu za kusikitisha za miaka aliyoipoteza katika himaya ya danguro la ‘msamaria.’
HISTORIA YAKE
Sara ni mmoja wa watoto watatu katika familia yao. Kaka  yake  Emmanuel Tarimo (31) na dada yake Neema Tarimo. Wakati akipochukuliwa na ‘msamaria’ alimuacha kaka yake huko Babati akijitafutia riziki kwa kubeba mizigo na dada yake akiendelea na masomo ya shule ya msingi.
Anasikitika kuwa katika maisha yake hakubahatika kumfahamu baba yake, lakini aliwahi kuelezwa na mama yake kuwa ni mwenyeji wa Kilimanjaro. Mama yake ndiye aliyekuwa anatunza familia yao licha ya  kwamba hakuwa na ajira rasmi, wala biashara za kudumu.
Mazingira hayo, yalimlazimisha kukatisha masomo  akiwa darasa la tatu katika shule ya Msingi Idangunyii. Anasema alikuwa na ndoto ya kupata elimu zaidi, lakini kifo cha mama yake kilisababisha ajione kuwa  hana bahati.
MAISHA KWENYE DANGURO
Alisimulia kuwa,  baada ya ‘msamaria ‘ kujitokeza na kumwahidi  kuwa atamtafutia shule na kugharamia elimu alimsikiliza na kumfuata hadi jijini  Dar es Salaam. Sara alieleza kuwa mwanamke huyo alipofika nyumbani kwao Babat, alieleza kuwa anatafuta wasichana 10  kwa ajili ya kufanya kazi za ndani kwa familia za  Dar es Salaam.
“Aliiambia  familia yangu kuwa, hata kama wasichana watakaopatikana watakuwa wanasoma wataendelezwa mara baada ya kufika mjini wakati wakiendelea na kazi ,’’ anasema na kuongeza:
“Nakumbuka ilikuwa siku ya Ijumaa mwaka 2003, tuliondoka kwa usafiri wa basi tukiwa 10 ingawa sikuwatambua wenzangu kwa sababu alituchukua kutoka katika vijiji tofauti.” Alisimulia kuwa walifika nyumbani kwa mwanamke huyo Mwananyamala Magengeni kwenye ghorofa mbili, ambayo juu linaonyesha ujenzi unaendelea.
Alisema wakiwa nyumbani kwa mama huyo, walibadilishwa mavazi kutoka yale waliyotoka nayo kijijini na kupewa nguo nyingine- sketi fupi, kaptula na  blauzi maarufu kama ‘vitop’.

Alikumbuka kuwa  baada ya kupewa nguo hizo, walitakiwa kila mmoja akajipumzishe kwenye chumba chake vilivyokuwa ghorofa ya kwanza.
 KUBAKWA MARA YA KWANZA
Alieleza kuwa siku hiyo akiwa chumbani kwake mlango uligongwa na alipouliza ni nani, alijibiwa na sauti ya kiume kuwa ni mlinzi. Alipofungua,  mwanaume mtu mzima alimwambia wakati huo sio wa kulala bali ni wa kazi na kumtaka avue nguo huku akimtisha na  bisibisi.
Vitisho  vilitawala akilazimishwa kufanya ngono kwa nguvu na  mwanaume huyo  aliyetumia bisibisi kumchoma  mdomoni  na mkononi  karibu na kiwiko.
“Nilipiga kelele za kuomba msaada lakini hakuna aliyekuja kunisaidia hadi yule mzee alipomaliza haja yake  na kuniacha nikiwa kwenye maumivu makali.”
Anasema  hakuamini kilichotokea na kulalamika kwa mwenyeji wake….“Nilimfuata yule mama kumweleza yaliyonitokea cha ajabu aliniambia hiyo ndiyo kazi niliyofuata mjini.”
Anasema “baada ya kupewa maneno hayo makali nilipelekwa  kwa daktari wa  hospitali ya Mwananyamala kwa uchunguzi zaidi.” Anasema aliendelea kuwa mtumwa wa ngono kwa sababu baada ya matibabu akawa anaendelea na kazi hiyo.
Sara anasema katika hospitali hiyo ndiko walikokuwa wanatibiwa na mwanamke huyo alimweleza kuwa huyo ni daktari wao. Anasema aliwahi kudhalilishwa kingono na wanaume zaidi ya 10  kwa siku moja, wakiwa wa rika, tabia  na maumbile  tofauti.

“Nakumbuka siku moja alikuja mteja aliyekuwa amelewa,  akaniambia amelipa fedha nyingi kwa mama na anachotaka ni kunitumia kinyume cha maumbile.”

“Sijawahi kufanya hivyo, nilipokataa alitoa kisu na kunitishia…alinilazimisha nivue nguo na kulala  kitandani kabla hajanijeruhi.” Anasema. “Nikiwa kitandani alidondosha kisu  tumboni mwangu, akakilalia na kunijeruhi, nikakimbizwa Mwananyamala na kutibiwa na yule daktari wa mwanzo niliyeambiwa ni  tabibu  wetu ambaye alinishona  sehemu nilizojeruhiwa na alikuja nyumbani kunitoa  nyuzi,” anasema MALIPO Sara anasema hakuwahi  kulipwa japo   wakati wakiendelea na kazi hiyo, mwanamke huyo aliwaeleza kuwa malipo yao ni Sh. 30,000 kwa mwezi na kwamba wangelipwa baada ya kukamilisha alichokitaka.
Akielezea faida waliyomtengenezea mama huyo alisema alikuwa akitoza kati ya Sh. 10,000 hadi 15,000 kwa wateja waliofanya ngono kwa njia ya kawaida na wale waliokuwa wakiwaingilia kinyume cha maumbile ilikuwa aliwalipisha  kati ya Sh. 30,000 na 50,000. Anaeleza kuwa walikuwa  wakipatiwa  matibabu, chakula na kununuliwa mavazi lakini hawakuruhusiwa kutoka nje ya nyumba hiyo. “Niliwahi kumhoji mama kwa nini alitudanganya unatuleta mjini kwa ajili ya kufanya kazi za ndani na kutusomesha?”
“ Nilimuomba anirudishe nyumbani, lakini alikataa na kuniambia kazi yake itakapokwisha nitarudi  sikuyaelewa majibu haya,” anasema.
ALIVYOTOROKA
Alisema baada ya kutumikishwa  kwa muongo mmoja, Februari 4, 2013,  siku  aliyofanikiwa kutoroka baada ya mwanaume aliyefanya naye mapenzi siku ya kwanza  kufika kwenye danguro hilo akihitaji huduma yake.
“Alilipia  na kuja chumbani kwangu na kunieleza kuwa lile embe lililokula kipindi kile  lilikuwa bichi, hivyo amekuja kwa mara nyingine  likiwa limeiva na baada ya kumaliza haja zake.”
“Aliniambia anataka kunipa zawadi hivyo niliporuhusiwa na mama tuliondoka naye, tukipita maeneo tofauti akinielekeza majina ya mitaa na mwishowe tuliingia sokoni Kariakoo,” anasimulia.
Waliondoka na gari aina ya Volkswagen  hadi Kariakoo na  wakati huo alihisi njaa  na kumuomba kabla ya  kumnunulia zawadi,  wanunue kwanza chakula.
Mteja huyo katika mazungumzo yake alimfahamisha kuwa ni mwanasheria anayefanya kazi manispaa japo hakutaja jina. “Tukiwa njiani alikokuwa amekusudia kunipeleka nilikuwa nikitembea nyuma yake,   hapo ndipo nilipotoroka nikikimbia bila kujua ninaelekea wapi, nilizunguka na hatimaye giza liliingia na watu walipungua kwenye eneo nililokuwapo.”
“Sijui ilikuwa saa ngapi, lakini  niliona gari la polisi niliamua kuwafuata nikamueleza askari wa  kike  mkasa mzima,” alisema. Anasema walikwenda kituo kikuu cha polisi na kuchukuliwa maelezo lakini pia alimpatia nguo nyingine kwa vile alikuwa amevaa mavazi yasiyo na staha.
 “Siku iliyofuata niliambiwa kuna dawati la kushughulikia masuala ya wanawake, lakini kwa wakati huo wahusika hawakupo. Ilipofika Alhamisi nilikabidhiwa kwa askari mwingine anaitwa Happy.”  Aliongeza: “tuliondoka naye hadi Oysterbay polisi, huko walitoka askari kadhaa kwenda  Mwananyamala nyumbani kwa  mama huyo.”
Sara alisema walifanya upekuzi kwenye vyumba walivyokuwa wakilala bila mafanikio, walishuka chini na kumuamuru afungue moja ya vyumba vilivyokuwa vimefungwa lakini mwanamke huyo alikataa na  polisi walimuagiza aende kituoni kuandika  maelezo dhidi ya  tuhuma hizo.
Alieleza kuwa wakati mtuhumiwa huyo akiwa mahabusu watoto wake anaoishi nao mmoja mwanaume mwenye  miaka 27 na mwingine wa kike walimsihi afute kesi hiyo, lakini alikataa na kuongeza kwa alifungua jalada la uchunguzi lenye kumbukumbu  RB/2468/2013  la Februari 7.
VYOMBO VYA HABARI
Alisema amefikisha suala hili kwenye vyombo vya habari akiomba msaada wa nauli ili aweze kurudi kwao pamoja na chakula. “Kabla sijafika NIPASHE nilitoa taarifa kwenye Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu ambacho kimeahidi kulifanyia kazi suala langu,” anasema.

AFYA YAKE
Sara analalamikia kuwa na vivimbe mbavuni  na sehemu za siri na anahofu kuwa huenda ameambukizwa magonjwa ya ngono na Ukimwi.
Anasema ana wasiwasi  kwa vile aliwahi kupata vipele vingi  mwilini japo  daktari wao alimueleza kuwa vilisababishwa na joto lakini sasa  vimekuwa uvimbe mkubwa. Anasema wakiwa kwenye danguro hilo daktari wao alikuwa anawapa dawa mara kwa mara ambazo hawafahamu zilikusudiwa kutibu nini na zilipomalizika aliendelea kuzileta japo hakuwahi kutumia tiba hiyo.
KONDOMU
Anasema baadhi ya  wanaume wenye ndoa walitumia kondomu wakati wa kufanya ngono lakini asilimia kubwa ya wateja wa danguro hilo walikuwa hawatumii mipira hiyo ya kiume. “Walikuwa wananiambia nina mke ninampenda hivyo natumia kondomu lakini wengine walikuwa hawatumii, chumbani tulikuwa tunawekewa kondomu lakini  ukiwaambia wazitumie wanakataa.”
KUGUNDULIKA NA VVU
Sara anasema Jumatatu Februari 11,  akiwa  polisi Oysterbay, aliamriwa kuondoka eneo hilo kwani si sehemu ya kuishi nail kufungua mashtaka. “Nilikwenda kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo lakini usiku nilizidiwa ilipofika  asubuhi nilikwenda zahanati ya Mwenge nilikotibiwa na kuelezwa kuwa nimeambukizwa Virusi Vya Ukimwi (VVU) na kutakiwa kuanza kutumia dawa.”
KULAWITIWA NA  POLISI
Wakati uchunguzi wa tuhuma dhidi ya Abia  ukiendelea, inadaiwa kuwa usiku wa Jumatano  polisi wa kituo cha Oysterbay alimlawiti Sara eneo lenye migomba kituoni hapo. Akizungumza na NIPASHE kwenye kituo cha trafiki kilichopo kituo cha mabasi ya mikoani Ubungo,  alisema  alifanyiwa unyama huo baada ya polisi kumfuata akiwa amelala kwenye maegesho ya magari.
Anasema alikwenda Ubungo kuchukua nguo  alizozificha hapo na akiwa huko alikutana na  askari huyo ambaye alimueleza matatizo yake, ndipo akamtaka wakale chakula.
“Baada ya chakula wakati tunarudi kituoni, aliniambia nimlipe kwa kumruhusu kunifanyia tendo hilo lakini nilikataa na askari huyo alinishika kwa nguvu na kunilawiti.” Anaongeza kuwa kutokana na kitendo hicho aliondoka kituoni hapo  saa 12:00 asubuhi na kufikisha taarifa ITV kwa vile aliona polisi hawakuwa na msaada kwake.
Baada ya kutoa malalamiko yake na kusaidiwa na wafanyakazi wa ITV alijitokeza  polisi mwanamke na kumchukua kwa matibabu kwenye zahanati ambayo Sara alisema haifahamu na baadaye kupelekwa kituo cha mabasi Ubungo ili kurudishwa nyumbani kwao Manyara. Alimweleza Mwandishi Wetu kuwa aliomba simu kutoka mtu aliyekuwa kituoni hapo ili awasiliane naye kabla hajasafirishwa na polisi hao.
Baada ya mwandishi kufika Ubungo na kufanya mahojiano na Sara gari la polisi   lenye namba PT 2083  lilifika na kumpeleka  polisi  Oysterbay  na kuandikisha  maelezo.
MAELEZO YA POLISI
Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kinondoni, John Mtalimbo,  alipofuatwa alisema taarifa zipo kwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya Kinondoni (OCD). Aidha, alisema kwa mujibu wa OCD msichana huyo amekuwa akitangatanga maeneo ya  Buguruni na sehemu nyingine ambazo hakuzitaja.
“Naona lengo lake ni kutuchafua, kwa nini asubuhi alikuja ITV na sio kutoa taarifa kwetu kama amelawitiwa na askari wetu, anatuchafua,” alisisitiza  Kamanda Mtalimbo. Alikiri kuwa siku mbili zilizopita polisi ilimtafutia tiketi ili kumrudisha kwao lakini haikufanikiwa.
Kamanda alipoulizwa sababu za kumsafirisha Sara wakati amefungua kesi ya kuuzwa kimwili  kwenye danguro alisema ni kutokana na kukosa makazi.  Awali, Mwandishi Wetu alinasa mawasiliano ya simu ya Kamanda Mtalimbo na mtu aliyeelezwa kuwa  ni OCD   akimwelekeza jinsi yakuandika maelezo dhidi ya binti huyo. Alisikika akisema: “Inabidi tujipange, hapa watakuja waandishi wa habari, (bila kujua kama mwandishi wetu alikuwepo eneo hilo), watataka kujua kinachoendelea na kumshauri andike kuwa walikubaliana kufanya ngono.”
Licha ya kusikia kilichozungumzwa juu ya mlalamikaji huyo  alipoingia ofisi kwake na   kujitambulisha  na kuuliza habari za Sara Mtalimbo alimweleza kuwa hana taarifa hizo na kwamba anasubiri zitoke kwa OCD.
Akisoma maelezo ya OCD wa Kinondoni,  Mtalimbo alisema Februari 2, mwaka huu Sara  aliripoti kituo hapo kuwa alikuwa akiishi Mwananyamala alikokuwa akifanyishwa kazi za kuuza mwili na mtuhumiwa aliyemtaja kwa jina la Abia.
Alisema baada ya polisi kupokea  malalamiko hayo  walikwenda Mwananyamala kuonyeshwa danguro hilo na polisi walipomkamata Abia mlalamikaji alishindwa kumtambua na kuongeza kuwa walifungua jalada la uchunguzi na kwa sasa mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana na Sara aliendelea kubaki kituoni hapo hadi alipoonekana ITV jana asubuhi.
Kamanda alielezwa kuwa katika mahojiano ya Sara na OCD alimfahamisha kuwa  Jumatano wiki hii akiwa Ubungo alitongozwa na askari aliyemuahidi kumpatia Sh. 10,000 baada ya kumlawiti.
“Walikwenda kwa makubaliano migombani na  baada ya kufanya kitendo hicho, askari alimpa Sh. 20,000 ,” alisema na kuhoji sababu za  msichana huyo kutofikisha  tukio hilo kituoni badala yake alikimbilia ITV. Hata hivyo alipoulizwa iwapo mlalamikaji amemtambua askari huyo kupitia gwaride la utambuzi na iwapo alichukuliwa hatua alisema bado na kuongeza:”Maelezo niliyokupa ndiyo mambo mengine yatafuata baadaye.”
NYUMBANI KWA ABIA
Gazeti hili likafika nyumbani kwa Abia na kukutana na  binti  alijitambulisha kuwa anafanyakazi za ndani na kueleza kuwa mwenye nyumba  hakuwepo na hajui alikokwenda. Alipoulizwa kuhusu danguro binti huyo mwenye miaka kati ya 13 na 20  alisema hafahamu kinachoendelea kwani mwajiri wake anamkataza kutoka nje kukutana na  majirani lakini akadokeza kuwa Jumatatu wiki hii walikuja polisi wakamkamata mama huyo ambaye  siku iliyofuata alirudi nyumbani.
KUWEPO MADANGURO
Majirani wa mtuhumiwa  walikataa kutoa ushirikiano kwa kuhofia wanazungumza na  polisi lakini Mwenyekiti Serikali ya Mtaa Kata ya Makumbusho, Said Muhunzi,  alisema uchunguzi uliofanyika umebaini kuwepo kwa danguro hilo.  “Nimebaini wapo wasichana wenye umri mdogo ambao wanaonekana na majirani wakiingizwa hapo kila mara na baadhi ya watu, majirani wamethibitisha hili,” alisema.
Aliongeza kuwa, Jumatano iliyopita kikundi chake cha ulinzi shirikishi, kilifika kwenye nyumba hiyo saa 7:00 usiku na  kumkuta mtuhumiwa Abia  na watu wengine wakiwa  nje na  kuwataka waingie ndani kwa kwani haukuwa  muda wa kukaa nje.  “Ijumaa iliyopita niliwaambia walinzi waende tena saa 8:00 usiku kuangalia kama watawakuta nje, waliona watu watano wakinywa pombe nje,” alisema na kuongeza:
Aliongeza kuwa watu hao ni Abia, Salome,  mtoto wa marehemu mumewe  na wanaume watatu na kuongeza kuwa kijana mmoja anayeitwa Juma alifahamika baada ya wenzake kumtaja kutokana na kuwatishia walinzi hao kwa bastola. Muhunzi alisema Salome  anatumiwa na Abia kutafuta mabinti kwa ajili ya danguro hilo na kwamba kufuatia tukio hilo la walinzi kutishiwa walifungua kesi tatu katika kituo cha polisi Minazini alizozitaja kuwa ni  kukutwa nje wakinywa pombe  usiku,kutishia kuua na  kuzuia ulinzi usifanyike
Alisema walifungua jalada lenye kumbukumbua RB/118/2013 na kesi hiyo ilifikishwa kituo cha polisi Oysterbay na kukuabidhiwa kwa mpelelezi aliyemtaja kwa jina moja la Mwesiga Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo, alisema eneo lake moja ya changamoto zilizopo ni kuibuka kwa madanguro na baadhi ya wasichana wenye umri mdogo kujiuza kwenye baa nyakati za usiku.
Alitaja baadhi ya baa (majina tunayo ) kuwa zinaongoza kwa kuwa na wasichana wengi wanaojiuza na kwamba wanatoa elimu kupitia kamati ya Ukimwi na kufanya msako lakini tatizo ni kubwa. Alitaja danguro maarufu liitwalo  ‘kwa wahaya’  lililopo Minazini na kusema kuwa  ofisi yake inawajua watuhumiwa kwa majina.
Habari zilizozifikia gazeti hili jana asubuhi, Sara alikuwa amewekwa mahabusu kituoni hapo.  
CHANZO: NIPASHE

No comments: