RELATIONSHIP/MAHUSIANO

NAKUJA KUZUNGUMZA NA VIJANA KATIKA UKURASA HUU KWA NIA YA KUELIMISHANA JUU YA MASWALA MENGI LAKINI HUSUSANI YANAYOHUSU UHUSIANO WETU NA WATU WENGINE.NAOMBA WAKATI UNASOMA HAPA UWE TAYARI KUJIFUNZA,KUTOA MAWAZO YAKO NA KUWA TAYARI KUBADIRIKA NA KUWAELEZA WENGINE. UNAWEZA PIA KUTOA USHAURI WAKO  CHINI YA MAKALA;MWISHONI KWA CHANI ITAKAYOWEKWA HAPA. KARIBU. KILA BAADA YA MAKALA NITAKUWA NAANDIKA JUU YA JAMBO ULILOLISOMA ILI UJIFUNZE SASA KUTOKANA NA YALE NITAKAYOKUWA NAYACHAMBUA KWA UNDANI KIONGOZI WETU IKIWA NI NENO LA MUNGU.


SABABU ZA UPUNGUFU WA MBEGU ZA KIUME

HALI ya maisha pamoja na mazingira husika yanayomzunguka binadamu imeelezwa kuwa ni chanzo cha kushuka kwa nguvu za kiume.
Madaktari  wengi wameripoti juu ya kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa wengi wa kiume ambao wamekuwa wakilalamikia juu ya upungufu wa nguvu za kiume.
Mwaka jana mwishoni  gazeti la The Independent llilopo nchini Uingereza  liliripoti kuwa hali ya afya ya viungo vya uzazi hususani kwa wanaume ilishuka kwa kiwango kikubwa na hiyo ilitokana na utafiti uliofanywa duniani juu ya ubora wa mbegu za kiume.
Utafiti huo ulionyesha kuwa katika miaka ya 1989 hadi 2005  ulionyesha kuwa kati ya wanaume 26,000 waliofanyiwa uchunguzi robo tatu yake walionekana kuwa na uwezekano mkubwa wa kushindwa kuzaa.
Mwaka  1989 na  2005, kwa mujibu wa gazeti moja la Uingereza lilisema kwamba  “Wanaume 26,000 wanakabiliwa na tatizo hilo la upungufu wa mbegu za kiume.’’
Utafiti huo uliendelea kufanyika ili kuhakikisha juu ya uchunguzi uliofanyika miaka 20 iliyopita na matokeo yake yalizidi kuonyesha kuwa nguvu za kiume zimezidi kudhoofika kwa wanaume wengi duniani.
Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikisababisha nguvu hizo kuporomoka ni pamoja na kuvaaji wa nguo za ndani ambazo zinabana, pia wataalamu  walieleza kuwa ufumbuzi juu ya sababu maalumu ya nguvu hizo kushuka bado haujapatikana.
Baadhi ya waandishi nchini Kenya  hususan katika gazeti la Daily Nation waliamua kufanya utafiti juu ya hilo ili kuweza kufahamu kama tatizo hilo lipo nchini humo.
Utafiti huo ulifanywa na daktari mmoja maarufu katika Hospitali ya Royal Garden nchini humo aliyejulikana  kwa jina la Solomon Wasike ambaye alisema kuwa wiki mbili zilizopita alipata mgonjwa mwenye tatizo kama hilo.
Aliongeza kuwa mwanamume huyo alikuwa na umri wa mika 28 alikuwa amefika katika kliniki yake kwa ajili ya kupima juu ya uwezo wake wa kuzaa.
Hali hiyo ilikuja baada ya kufunga ndoa na mke wake mwaka mmoja uliopita lakini hadi sasa mwanamke huyo alishindwa kupata mimba.
Daktari Wasike alisema kuwa baada ya maelezo hayo aliamua  kuchukua mbegu zake mwanaume huyo  kwa ajili ya vipimo aliongeza kuwa majibu yake yalikuwa na utata kwa kuwa yalionyesha kuwa mtu huyo alikuwa na uwezo mdogo wa kuzalisha mbegu hali ambayo iliyosababisha mke wake kutopata mimba.
Wasike alisema kuwa hali hiyo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika kliniki hiyo kuwa na wagonjwa wengi wa kiume wenye matatizo katika afya ya uzazi.
“Kinachotusumbua ni kwamba vijana wengi wanaokuja katika hospitali  hii wamekuwa na matatizo sawa katika mbegu za kiume na jambo hili linazidi kusikitisha kwa kuwa asilimia kubwa ya watu wanaokuja ni vijana.
Aliongeza kuwa hali hiyo inafanya tuamini kuwa licha ya wengine kuwa na matatizo hayo tangu kuzaliwa lakini asilimia kubwa ya vijana wanapatwa na tatizo hilo kwa sababu ya  hali ya maisha wanayopitia pamoja na mazingira wanayoishi.
Hata hivyo takwimu za kitaifa bado hazijafanywa  juu ya tatizo licha ya kuwa kumekuwa na malalamiko mengi ya wanaume kutoka katika katika hospitali mbalimbali.
Pia kuna takwimu kutoka katika kituo cha afya Nairobi IVF Centre, ambacho ni mojawapo kati vituo ambavyo uhusika na upimaji wa mbegu za kiume kwa kiasi kikubwa ambao nao pia waleleza kuwa kiwango kidogo cha mbegu za kiume ambazo pia huwa ni dhoofu  kimezidi kujitokeza kwa baadhi ya wanaume wengi nchini humo.
Dk Joshua Noreh ambaye alikuwa anahusika na upimaji pamoja na utoaji wa huduma katika kituo hiko alisema kuwa wastani wa wanaume ambao wanatembelea katika kituo hiko huwa na umri wa miaka 35.
Aliongeza kuwa kwa mujibu wa data kutoka katika kituo chake asilimia 14 ya wanaume ambao mbegu zao zilifanyiwa utafiti zilionyesha kuwa wamekuwa na tatizo  hilo.
Aliongeza kuwa hali hiyo imezidi kwa asilimia tatu.
Miaka mitatu iliyopita asilimia 11 ya wanaume walionekana kuwa na tatizo hiyo hali ambayo imeonyesha kuwa tatizo hilo limekuwa likikua kila baada ya mwaka mmoja.
Kwa mujibu wa maelezo kutoka Shirika la Chakula Duniani (WHO)  lilieleza kuwa mwanamume mwenye mbegu za kiume ambazo hazina matatizo anatakiwa  awe na mbegu za kiume kuanzia milioni 10 hadi 20 kwa milimita.
Tatizo hilo la kuwa na mbegu za kiume ambazo ni dhoofu zinazosababisha kutokuwa na uwezo wa kuzaa husababishwa na kubadilika kwa hali ya maisha pamoja na kubadilika kwa mazingira.
Daktari huyo aliwataka wanaume kuwa makini na maisha ambayo wanaishi kwa kuwa yanaweza kuathiri utendaji kazi wa mbegu hizo.
Pia aliwataka wanaume kupunguza uvutaji wa sigara pamoja na unywaji wa pombe kupitiliza, kula vyakula vya kukaanga vyenye mafuta kwa kuwa vinaongeza  kwa kiasi kikubwa tatizo la kushindwa kuzaa.
Utafiti uliofanywa mwaka 1940 ulionyesha kuwa asilimia 50 ya nguvu za kiume hushuka kutokana na kiwango kikubwa cha unywaji wa uvutaji wa sigara, pombe pamoja na mabadiliko ya mazingira.
Pia uvutaji wa sigara 20 kwa siku na ulaji wa chipsi, baga, soseji inachangia kwa asilimia 43 kuharibu nguvu za kiume.
Dk Wasike alisema kuwa asilimia kubwa ya wanaume wanaosumbuliwa na tatizo hilo kutokana na hali ya mazingira wanayoishi ni wale ambao wanafanya kazi shambani kwa kuwa kuna aina ya madawa ambayo yanapulizia yanaharibu mbegu hizo.
Pia aliongeza kuwa wanaume ambao wanaendesha vyombo vya moto na kukaa karibu na injini hizo za magari na wale ambao wanapakata kompyuta katika mapaja kwa muda mrefu wanahatari kubwa ya kupata tatizo hilo.
Aliwataka wanaume kula mboga za majani kwa wingi na matunda na kupunguza ulaji mkubwa wa nyama na maziwa kwa kuwa hivyo pia ulichangia tatizo hilo.
Vilevile aliwataka wanaume kula vyakula vyenye virutubisho ambavyo vitasaidia katika kujenga mwili ikiwemo na kuvipa uwezo mbegu hizo.
Wanaume pia walitakiwa kuacha kuoga kwa kutumia maji ya moto kwa kuwa hupunguza uwezo wa kutengeneza nguvu zao.
Alishauri pia kama mwanamume anapenda kuongeza nguvu za kiume mwilini mwake anatakiwa apunguze kuvaa nguo za ndani ambazo zinabana na badala yake kuvaa zinazoachia ili kuwezesha mwili kupata hewa.
Ili kupunguza tatizo hilo hususan kwa vijana walitakiwa kupunguza kula mirungi kwa sababu ni hatari katika viungo vya uzazi vya mwanamume yeyote ambaye anapenda afya yake.
Wasike ilisema kuwa wananchi wengi wamekuwa wakidharau kula maharage ya soya, lakini kwa upenda wake alisisitiza kuwa anawashauri watu kupendelea kula maharage ya soya kwa kuwa yana virutubisho aina ya estrogen ambavyo huzalisha aina ya virutubisho vya testosterone vinavyosaidia katika uzalishaji wa mbegu za kiume.
Pia kwa mujibu wa tafiti mbalimbali walibaini ya kuwa Kuna aina mbili  ya vyakula ambavyo vilifanyiwa utafiti na kubaini kuwa ni moja ya vyakula vilivyosaidia kuongeza nguvu za kiume na havina madhara katika engezeko la nguvu za kiume.
Miongoni mwa vyakula hivyo ni pamoja na tangawizi ambapo walieleza kuwa huweza kuliwa ikiwa imechemshwa ambapo wengine huifanya kama ni chai.
Pia tangawizi hiyo inaweza kuchanganywa na vitu asilia mfano  wa kiasili kwa kutumia asali, kitunguu saumu ama tangawizi yenyewe.
Aina ya pili ni tunda la Tikiti maji ambapo linaweza kuliwa kwa kutengenezwa kama juisi au linaweza likaliwa lenyewe kama tunda.
Kutokana na kuwapo kwa tatizo hilo la upungufu wa nguvu za kiume nchini Kenya  waliamua kufungua mtandao wa masuala ya afya ya uzazi ili kuwawezesha kutoa mafunzo mbalimbali juu ya tatizo hilo.
Kiongozi wa masuala ya afya ya uzazi nchini humo, Dk Isaack Bashir alisema kuwa mtandao huo pia utatoa fursa kwa wataalamu mbalimbali kuelezea juu ya afya ya uzazi.
Alisema kuwa mtandao huo ulifadhiliwa na USAID  wakisaidia na FHI pamoja na Wizara ya Afya kwa ajili ya kufanikisha mpango huo.

Mwananchi: Jumatano Februari 27,  2013

No comments: