NYUMBA NYINGI KUPOROMOKA NCHINI
Baadhi ya majengo ya ghorofa yaliyopo jijini Dar es
Salaam
Na Aidan Mhando,
Mwananchi
Posted
Aprili27 2013 saa 23:40 PM
Pia, hatua hiyo inatokana na kutokuwapo kwa ukaguzi
wa vifaa mbalimbali vya ujenzi yakiwamo matofali ya saruji yanayotumika katika
ujenzi wa nyumba hizo.
Uchunguzi uliyofanywa na Mwananchi hivi karibuni
jijini Dar es Salaam na baadhi ya maeneo nchini, umebaini kuwepo kwa ongezeko
kubwa la biashara holela ya matofali yanayotengezwa kwa ubora hafifu.
Uchunguzi pia unaonyesha kutokuwapo kwa usimamizi
wa kutosha katika sekta ya ujenzi nchini ni moja ya vyanzo vya watu kufanya
biashara ya vifaa vya ujenzi kiholela.
Biashara hizo ni pamoja na uuzaji wa matofali yasiyokuwa na viwango kutokana na kukosa udhibiti maalumu.
Moja ya mambo yanayosababisha matofali yanayotumika
katika ujenzi jijini Dar es Salaam kuonekana kuwa hayana ubora ni utengenezaji
wa matofali hayo.
Imegundulika kuwa saruji inayotumika katika
utengenezaji huo ni ndogo na mchanga unakuwa mwingi kwa lengo la kutengeneza
matofali mengi ili kupata faida.
Wakati uchunguzi huo ukionyesha hivyo Mwananchi,
ilimtafuta Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), Mhandisi Boniface
Muhegi, ambaye alishauri kufanyika kwa uchunguzi wa bidhaa zinazotumika katika
ujenzi.
Muhegi anasema “Ili kuepusha madhara hasa kuanguka
kwa majengo ni vyema Shirika la Viwango Tanzania (TBS), likachukua hatua ya
kufanya ukaguzi wa vifaa vinavyotumika kwenye ujenzi ili kuongeza usalama
katika masuala ya ujenzi.
Anasema ili kuhakikisha kuwa majengo yanakuwa
salama, ni vyema watu wakatumia wakandarasi waliosajiliwa ili kuwabana wakati
kunapotokea madhara.
“Sisi tunashauri kwamba kama mtu anataka kujenga
nyumba amayo ni salama, ni vyema akatumia wakandarasi waliosajiliwa ili iwe
rahisi kuwabana wakati tatizo lolote linapojitokeza,”anasema.
Mhandisi Muhegi anasema “Ni vyema wananchi nao wakatambua
kwamba matumizi ya vifaa visivyokuwa na viwango sio salama kwa maisha yao”.
Anasema kila mmoja aone haja ya kutumia vifaa
vyenye ubora ili kujihakikishia usalama wa makazi yake na kuepusha kutokea kwa
majanga mbalimbali.
Kama
tutakuwa makini katika matumizi ya vifaa bora vya ujenzi tutakuwa na makazi
salama na tutaepusha majanga mbalimbali.
NUKUU:
Machi
29 mwaka huu jengo la ghorofa 16 liliporomoka jijini Dar es Salaam na
kusababisha vifo vya watu zaidi ya 30.
Febuari
17 mwaka huu, jengo lingine la ghorofa tatu liliporomoka huko Sinza Mori Dar es
Salaam na kusababisha kifo cha mtu mmoja na wawili waliokolewa na vikosi vya
uokoaji.
Mwaka
2006 Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliunda tume ya kufuatilia ujenzi wa maghorofa
na kubaini kuwa zaidi ya majengo 100 jijini Dar es Salaam yamejengwa bila
kuzingatia vigezo.
Msomaji
wetu kama una maswali yoyote kuhusiana na ujenzi na ubora wa majengo unaweza
kumuuliza Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB), kwa kutuma kupitia
baruapepe:
mwananchijumamosi@yahoo.com au ujumbe wa simu kupitia namba: 0658 376410
CHANZO:
MWANANCHI 28/04/2013
No comments:
Post a Comment