Sunday, December 23, 2012

UZINDUZI WA KITABU CHA MWL PROSPER ULIKUWA HIVI

Hatimaye uzinduzi wa kitabu cha mafundisho ya namna ya kumlea mtoto na kijana wako kimezinduliwa Jumapili ya tarehe 9 Desemba, 2012. Ibada ya uzinduzi wa kitabu hicho ulifanyika katika kanisa la city Haverst, katika ibada hiyo ambayo mihubiri wake alikuwa mtunzi wa kitabu hicho mwl Prosper. kitabu hicho kiwekwa  wakfu na kuzinduliwa na Mch kiongozi wa kanisa hilo Mch Yaled Dondo aliyeshiriki katika kuandika DIBAJI. Mambo yaliyomo kwenye kitabu hicho ni kama ifuatavyo.

 YALIYOMO

UTANGULIZI

SURA YA KWANZA (1)

HATUA ZA MAKUZI YA MTOTO

HATUA YA KWANZA

HATUA YA PILI

HATUA YA TATU

SURA YA PILI (2)

MATATIZO YA WATOTO NA VIJANA

SURA YA TATU (3)

AINA ZA MALEZI KATIKA MALEZI YA MTOTO

A. MALEZI YA KUTUMIA MAMLAKA AU NGUVU

MADHARA YA KUTUMIA MAMLAKA NA NGUVU.

B. MALEZI YA KURUHUSU (LAISSEZ FAIRE)

C. MALEZI YA KIDEMOKRASIA

D. MCHANGANYIKO WA MALEZI

SURA YA NNE (4)

MAZINGIRA YA MTOTO

A. MAZINGIRA YA NYUMBANI

A. MAZINGIRA YA SHULENI

B. MAZINGIRA KATI YA NYUMBANI NA SHULENI

SURA YA TANO (5)

WAZAZI WAFANYE NINI KWA WATOTO WAO


 kitabu hicho kitakazoanza kupatikana sehemu mbalimbali vinakouzwa vitabu si cha kukosa maana kina mafundisho ya muhimu yanayohusu kuzitambua tabia za watoto wetu na namna ya kuwalea. katika kipindi tulicho nacho kumekuwa na mmomonyoko wa maadili ambayo imekuwa ni changamoto kubwa kwa kanisa na taifa kwa ujumla lakini mtumishi huyu wa Mungu amekuja na mafundisho ambayo yataisaidia jamii kuweza kupunguza mmomonyoko huo wa maadili ambao umesha kuwepo katika jamii.

Watoto wakihudumu katika ibada hiyo

Mch Kiongozi Yaledi Dondo akiwa ameshika vitabu

Sehemu ya watu waliohudhulia ibada hiyo

Vitabu vikifunguliwa

Vitabu tayari vimesha funguliwa

Mch Yaledi Dondo kushoto pamoja na Mr&Mrs Willbroad

Mch Yaledi Dondo kushoto pamoja na Mr&Mrs Willbroad

Wanafamilia walioambatana na mwl Prosper.
Mwonekano wa kitabu kwa nje
 

No comments: